Wema Sepetu Amuingiza Matatani Mchungaji


Mchungaji David Mashimo ambaye alitangaza kuendesha maombi ya kumuombea mrembo Wema Sepetu, amesema kitendo hicho kilimgharimu na kupelekea viongozi wa kanisa lake kumjia juu.

Akizungumza kwenye Friday Nigh Live ya East Africa Television, Mchungaji Mashimo amesema kwamba  baada ya yeye kutangaza mkesha wa kumuombea Wema Sepetu, viongozi wake walimzuia na kumtaka kuchagua kutoka kanisani hapo au kuacha kumuombea.

“Vikwazo ambavyo nilivipata, Mungu alivyonipa maono kwa ajili ya Wema Sepetu, nilivyotangaza ule mkesha kwamba ni mkesha wa maombi ambao ndani yake kuna toba kwa ajili ya Wema Sepetu, viongozi wangu wa dini walinizuia, wakaniambia inakuwaje unamuombea mtu ambaye si sahihi, mtu asiyefaa, na vile vile walitoa maneno makali kwamba kahaba, kitu ambacho hakipo”, amesema Mchungaji Mashimo.

Mchungaji aliendelea kwa kusema kwamba ….. “wakaniambia nichague mawili, kwamba mkesha ufanyike au usifanyike,  kwa kuwa nilitumwa na Mungu, na Wema Sepetu ni mtoto wake, anastahili haki za Kiungu kama wanavyostahili watu wengine, nikaamua kuachia kanisa na ule ukumbi, nikarudi kumtumikia Mungu chini ya mti, sasa hivi ninafanyia ibada chini ya mti, na watu wangu alionipa Mungu”.

Baada ya tukio hilo Mchungaji Mashimo amesema kwamba kitendo cha viongozi wake wa kanisa kumkataza kumuombea Wema Sepetu kilimuuma sana, kwani naye ana haki kama wengine.

“Kitendo hiki nikashangaa sana, kwa sababu Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea, kiongozi wa dini kusema kwamba Wema hafai, kiliniuma sana”, amesema Mchungaji Mashimo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad