Yanga Wakifikisha Nusu ya Mashabiki Tuliokua Nao Jana Najiuzulu Nafasi Yangu- Haji Manara

Yanga Wakifikisha Nusu ya Mashabiki Tuliokua Nao Jana Najiuzulu Nafasi Yangu- Haji Manara
Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara ameendelea na majigambo yake hasa kwa watani wake Yanga, ambapo amesema kuwa endapo watani zake wa jadi Yanga katika mchezo wake na Tukuyu Stars leo, wakifikisha nusu ya mashabiki waliohudhuria kwenye mchezo wao dhidi ya Nkana FC, yuko yatari kujiuzulua nafasie ya usemaji, ndani ya klabu.

Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika kuwa Simba haiwezi kufananishwa na timu zingine Tanzania wakiwemo watani wake, Yanga.

"Yanga leo wanacheza na Tukuyu Stars, wakijaza asilimia kumi kama jana najiuzulu usemaji wa Simba, halafu yupo mswahili anaweza kuthubutu kunifananisha De la boss na wasemaji wengine?", ameandika Manara.

Yanga inacheza na Tukuyu stars katika dimba la taifa, jijini Dar es salaam katika michuano ya shirikisho (AFC), huku watani wao Simba wakiwa  wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15, wakiichapa Nkana FC ya Zambia.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad