Yanga Yapania Kumaliza Mbeya City

Yanga Yapania Kumaliza Mbeya City
BAADA ya watani zao Simba kutolewa kwenye hatua ya tatu kwenye kombe la Shirikisho na kikosi cha Mashujaa kutoka mkoani Kigoma, Yanga wamesema wanataka kuwa mashujaa kwa kuwafunga Mbeya City katika mchezo wao kesho.

Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema wachezaji wote 20 ambao wapo Mbeya wana hali nzuri na wapo tayari kupambana kutafuta matokeo kwenye mchezo wao utakaochezwa uwanja wa Sokoine.

"Tupo sawa na tunaendelea vizuri na maandalizi, tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na ushindani uliopo ila tunataka kuendeleza rekodi yetu ya kutofungwa na kufanikiwa kuchukua pointi tatu ili tuwe mashujaa wa mchezo," alisema.

Mashujaa kutoka Kigoma inashiriki Ligi Daraja la kwanza ilifanikiwa kuisukuma Simba kwenye michuano ya FA katika uwanja wa Taifa kwa kuichapa mabao 3-2.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad