Zitto Kabwe Aeleza Hofu Yake Baada ya Kutoka Takukuru


Zitto Kabwe Aeleza Hofu Yake Baada ya Kutoka Takukuru
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amesema ana hofu kuwa maelezo yake aliyoyatoa TAKUKURU yanaweza yasitumike kusaidia kuondoa tatizo la rushwa.

Zitto ameweka wazi hilo baada ya kutoka kufanya mahojiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),  ambayo ilimuita baada ya kutoa madai kuwa kuna rushwa inafanyika kwenye uagizaji wa bidhaa za chuma nje ya nchi.

''Nimewaeleza tangu mwanzo kuwa nina wasiwasi, pamoja na kwamba wamekuwa wakitimiza wajibu wao kitu ambacho ni jambo zuri lakini hofu yangu ni kwamba isije ikawa kuniita kwao ni kujaribu kuzima jambo hili na sio kufuatilia'', alisema Zitto.

Aidha Zitto amesema amewapa changamoto TAKUKURU ya kushughulikia malalamiko ambayo yapo ya uagizwaji wa bidhaa za chuma nje ya nchi wakati kuna viwanda vinazalisha hapa nchini.

Disemba 1, 2018, TAKUKURU ilimuita Zitto kwa lengo la kutaka kudhibitisha madai yake ya uwepo wa kampuni tatu za Chuma kutoka China, Urusi na Uturuki ambazo zimewahonga watendaji wa Wizara za Fedha na Viwanda pamoja na Ofisi ya Rais kwaajili ya kuchelewesha mradi wa Mchuchuma na Liganga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad