Zitto Kabwe Awasilisha Ushaidi Takukuru

Zitto Kabwe Awasilisha Ushaidi Takukuru
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amewasilisha vielelezo vya ushahidi katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Maelezo hayo ni kuhusu madai yake ya kampuni tatu za chuma kuwahonga baadhi ya viongozi wa Serikali.

Baada ya kauli yake hiyo,  Takukuru ilimuomba mbunge huyo afike ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ili kushirikiana kushughulikia suala hilo muhimu.

Katika mitandao ya kijamii Zitto anadaiwa kuandika kuwa amepata habari za kushtua kuwa kampuni tatu za China, Urusi na Uturuki zimewahonga baadhi ya watendaji wa Serikali kuchelewesha  mradi wa Mchuchuma na Liganga, lengo ni kuhakikisha nchi hizo zinapata soko la chuma chao.

Akizungumza leo baada ya kuwasilisha maelezo yake amesema, “Baada ya kupata taarifa hizo niliwaeleza kuwa ninaweza kufika leo. Nimefika na nimetoa maelezo ya sababu ninazoziamini za ucheleweshaji wa mradi huo kuwa ni za makusudi na zimefanywa na Serikali.”

Amesema ucheleweshaji huo ni kwa ajili ya kunufaisha kampuni zinazoingiza  bidhaa zinazotumika kwenye miradi ya chuma kama kampuni zinazojenga reli ya kati na kuagiza chuma kutoka nje badala ya kutoka ndani ili kukuza uchumi.

“Mradi wa Mchuchuma na Liganga ungekuwa umeanza mkandarasi asingeagiza chuma kutoka nje angenunua hapa ndani hata kwenye mradi wa bomba la mafuta mkandarasi naye angefanya hivyo.”amesema

Amesema baada ya maelezo yake hayo ameiomba Takukuru kuendelea kuchunguza uagizaji wa bidhaa za chuma ambazo viwanda vya ndani vina uwezo wa kutengeneza, lengo likiwa ni kupata ukweli wa jambo hilo na kwamba kesho atawasilisha tena maelezo yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad