TIMU ya Azam FC imerejea jijini Dar es Salaam, mapema leo baada ya jana (Jumapili) kuibuka na ubingwa wa Mapinduzi Cup kwa mara ya tatu mfululizo katika mchezo wao dhidi ya Simba uliopigwa katika Uwanja wa Gombani Visiwani Pemba na kufanikiwa kuwachakaza Simba mabao 2-1.
Baadhi ya mashabiki wa Azam FC, wakishangilia baada ya timu yao kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa zamani mapema leo
Wakati huohuo, wachezaji na benchi la ufundi la klabu ya Simba lililokuwa Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mapinduzi wamerejea jijini Dar es Salaam, mapema leo kwa ajili ya kujiandaa na michuano mengine ambapo jana walipoteza mchezo wao wa fainali dhidi ya Azam FC,