MWANAMUZIKI wa Marekani, Christopher Maurice Brown maarufu kama Chris Brown, ameachiwa huru na polisi bila dhamana jijini Paris, Ufaransa, baada ya kukamatwa na kuhojiwa leo, Januari 23, juu ya tuhuma za mwanamke wa Ufaransa aliyesema amembaka.
Baada ya kuachiwa msanii huyo alikanusha taarifa za mwanamke huyo kuhusiana na kumfanyia tukio hilo huku post hiyo ikiandamana na picha iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka ‘This Bitch Lyin’.
“Nataka kuweka mambo sawa, huu ni uwongo, huku ni kunivunjia heshima kwa mwanangu na familia yangu kwa hadhi niliyonayo” aliandika Breezy kwenye akaunti yake ya instagram.
Mwanasheria wa Chris Brown amefunguka na kusema kwamba madai yaliyokuwa yanamkabili msanii huyo si ya kweli, ni uongo mtupu.
Chris Brown anaruhusiwa kuondoka Ufaransa muda wowote kuanzia sasa kwa sababu hana kesi inayomkabili