Msanii wa kike wa muziki nchini Afrika Kusini, Sho Madjozi ambaye anatamba na wimbo wa Kiswahili unaojulikana kwa jina la 'Huku', ameitaja siri iliyomfanya hadi kuimba wimbo huo.
Madjozi ameimba wimbo huo kwa mashairi ya Kiswahili, hali iliyopelekea watu wengi kushangazwa na uwezo wake wa matamshi ilhali sio raia wa nchi za Afrika Mashariki ambazo zinatumia zaidi lugha hiyo.
Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Twitter, Madjozi ameandika kuwa familia yake ilihamia kuishi nchini Tanzania mwaka 2008, jambo liliomsaidia kukuza ujuzi wa lugha hiyo na kutoa wimbo wake mwaka uliopita.
In 2008 my family moved to Tanzania, which is why in 2018 I was able to release a song in Kiswahili #2008vs2018 💖 pic.twitter.com/79DV0SX214— #LimpopoChampionsLeague (@ShoMadjozi) January 14, 2019
Wimbo huo uliachiwa mwezi Mei, 2018 ambapo katika Youtube umetazamwa mara milioni 3.3 na kuufanya kuwa maarufu nchini Afrika Kusini.