Abdallah Hamisi: “Ligi ya Kenya inaushindani kuliko Tanzania”
0
January 29, 2019
Mtanzania Abdallah Hamisi anaechezea Bandari FC ya Kenya ametofautisha ligi ya Kenya na Tanzania kwa kusema, ligi ya Kenya ina ushindani na timu yoyote inaweza kuwa bingwa tofauti na Tanzania ambapo timu chache ndio zinapewa nafasi ya kuwa bingwa wa ligi kuu.
“Mpira ni uleule lakini Tanzania na Kenya kuna utofauti kidogo, Kenya kuna ushindani wa kila timu kushinda ligi lakini Tanzania ni timu mbili labda ikipambana sana Azam.”
“Simba na Yanga ndio zinabadilishana ubingwa wa ligi ya Tanzania timu nyingine hazina usindani tofauti na Kenya ambako kuna Tusker, Gor Mahia, Bandari, Ulinzi timu kibao zenye nguvu ya kuchukua ubingwa.”
KUHUSU KUIFUNGA SIMBA KWENYE SPORTPESA CUP
“Mimi na wachezaji wenzangu wa Bandari tunashukuru kukutana na timu kubwa kwa sababu sasa hivi Bandari tunakwenda kucheza mechi za kimataifa kwa hiyo ni lazima tupate timu mechi kubwa.”
“Tulikuwa tunatamani kukutana na timu kama Simba, Yanga tofauti na Gor Mahia na Leopards ambazo tunazifunga kwenye ligi.”
HAONEKANI TAIFA STARS SHIDA NINI?
Kipindi cha nyuma alikuwa anapata nafasi ya kuitwa timu ya taifa na kucheza kikosi cha kwanza lakini kwa sasa hatumuoni wakati anafanya vizuri akiwa na Bandari FC.
“Shida ilikuwa ni moja, nilipotoka Sony Sugar kwenda Bandari FC kulitokea mvutano kidogo kwa hiyo kibali changu cha kazi kikawa kimechelewa halafu timu ya taifa inahitaji mtu ambaye anacheza mara kwa mara kwa sababu anakuwa fit kwa hiyo labda walivyoniangalia wakakuta sipo vizuri lakini naamini wachezaji wanaotuwakilisha ni wazuri kwa hiyo nafasi ikitokea nitarudi tena timu yataifa.”
KUNA OFA YOYOTE AMEPATA TOKA TIMU ZA TANZANIA?
“Zipo lakini mimi siwezi kuzungumzia sana jambo hilo, wakala wangu ndio mwenye taarifa sahihi zaidi kuhusu mambo hayo.”
Tags