Msanii Abdukiba ambaye leo, Januari 17 amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Omari Salehe, ameweka wazi matatizo aliyoyapata baba yake, yaliyopelekea hadi kifo chake.
Akizungumza na Big Chawa wa East Africa Radio, Abdukiba amesema kwamba baba yake alipata stroke ya kichwa, ugonjwa uliomsumbua kwa muda mrefu hadi kupelekea kulazwa ICU kwa wiki mbili, mpaka leo umauti ulipomkuta.
“Alikutwa na matatizo ya stroke ya kichwa kwa sababu alikuwa ni dereva wa mabasi ambayo yanasafiri ndani ya nchi na nje ya nchi, kwa kipindi kirefu amefanya hizo kazi nadhani ndiyo zimemsababishia maradhi ya yeye kupata stroke, tumejitahidi kumuhudumia, amekaa ICU almost wiki mbili, so mpaka kufikia hivi leo”, amesema Abdukiba.
Abdukiba ameendelea kusema kwamba msiba upo nyumbani kwao Kariakoo, na mazishi ya baba yake yatafanyika leo jioni, kwenye makaburi ya Kisutu.
Mzee Saleh alikuwa ni baba mzazi wa msanii Abdukiba, Alikiba na dada yao Zabibu Kiba.