ACT Wazalendo Waishauri Serikali ya Tanzania Kuiga Mfano wa DRC

ACT Wazalendo Waishauri Serikali ya Tanzania Kuiga Mfano wa DRC
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amezitaka asasi za kiraia, Makanisa pamoja na wanaharakati wote kuungani ili kuindoa CCM madarakani mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu.

Ado ameyasema hayo siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais wa upande wa upinzani huko Congo-Kinshasa, Bw. Felix Tshisekedi kutangazwa kuwa mshindi.

Ado amesema kwamba kitendo cha mpinzani Tshisekedi kushinda Urais ni kutokana na raia wa Congo kuungana pamoja kutaka mabadiliko na siyo kuviachia vyama peke yao.

"Kanisa Katoliki kule Congo lina nguvu kubwa sana ya ushawishi. Asasi za kiraia zilikubali kuungana na kutetea maslahi ya Umma. Hapa kwetu Makanisa yakikemea tu yanaambiwa wanafanya siasa. Upinzani wote tukiungana naamini 2020 CCM haichomoki.

Mbali na hayo Ado amewapongeza upinzani wa Tanzania kuungana mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu jambo analoliamini kwamba litawapa muda wa kujdiliana na kumpata kiongozi mmoja atakayeungwa mkono katika mbio za Urais.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad