Nilifukuzwa kazi miezi minne baada ya kupewa likizo ya uzazi.''
"Nilikuwa tegemeo la familia yangu, sikua na muongozo wa sheria kwa hiyo nilishauriwa kutia saini 'mkataba wa lazima', Nilijihisi mnyonge sana."
Haya ni maneno ya mama aliyezungumza na BBC baada ya kuchapisha makala kuhusu haki wa wanawake wajawazito kazini.
Kisa chake - na visa vya wengine wengi- vinaashiria ubaguzi unaoendelea kuwakabili wanawake wanaofanya kazi katika makampuni makubwa ya Ungereza ambapo viongozi wa ngazi ya juu wanakiuka sheria na kuwanyanyasa wanawake wanaopata ujauzito wakiwa kazini.
Lakini waathiriwa wanahofia sana kuzungumza kwasababu wamelazimishwa kutia saini mkataba wa kutozungumzia masaibu yanayowakabili.
Katika visa vingine masharti hayo yanawatishia kutozungumzia hali zao kwa ''pamoja''
"Masharti hayo yanaziwezesha makampuni kuvunja sheria," alisema mama aliyewasiliana na BBC.
"Unahitaji kuwa mjasiri na mvumilivu sana kushinda kesi mahakamani.''
"Nilikuwa na mtoto mchanga na wakati huo pia nilikuwa na hofu kuhusu jinsi nitakavyolipa deni la nyumba kwa hivyo sikuweza kupambana na kesi.
Karibu miaka tano sasa, baada ya kufutwa kazi katika mazingira ya kutatanisha anasema: "Tafadhali usichapishe jina langu, nataka kuangazia kisa changu tu. Nataka sheria ifanyiwe mabadiliko. Hii iliyopo haiwapatii ulinzi wanawake hata kidogo."
Sheria iko wazi: ni kinyume cha sheria kufuta mtu kazi kwasababu ni mjamzito au yuko likizo ya uzazi.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Lakini wanawake wanaendelea kunyanyaswa. Ni hivi majuzi tu waziri wa biashara Kelly Tolhurst, alisema: "Ubaguzi dhidi ya wanawake wajawazito na wale waliyo likizo ya uzazi ni ukikaji wa sheria, lakini baadhi ya kina mama wapya wanashindwa kuendelea na kazi hata wakirudi kutokana na mazingira magumu ya kazi ambayo inawalazimu kuondoka."
Mwanamke mwingine aliyewasiliana na BBC alijifungua miezi michache iliyopita na yeye pia hakutaka jina lake litajwe.
Masaibu yake yalianza pale bosi wekea alipomuita kujadali masuala ya kazi na mipango yake ya baadae.
"Nilipomwambia kuwa niko mjamzito alibadilika ghafla na kutoka wakati huo mtazamo wake kwangu ulibadilika kabisa, hilo lilinishangaza sana." alisema.