Airport Yajibu Tuhuma za Kuibwa kwa Vitu vya Abiria Zilizotolewa na Ray

Airport Yajibu Tuhuma za Kuibwa kwa Vitu vya Abiria Zilizotolewa na Ray
Uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umewataka abiria wanaodhani wamepoteza vitu vyao wakati wanasafiri kwa kutumia Uwanja huo watoe taarifa mapema ili waweze kusaidiwa kupata vitu vilivyopotea.



Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Paul Rwegasha amesema iwapo mtu atapata tatizo lolote ni vyema akawasiliana na uongozi badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwani atakuwa anaichafua nchi.


Rwegasha amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya uwepo wa taarifa za Msanii Maarufu wa Filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akieleza aliibiwa vifaa vyake akiwa anaelekea Dubai.



Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wakati uliopita pia kuna mama mmoja aliibiwa alivotoa kwenye media jibu likawa kali kwake kwa nini ametoa kwenye media sasa mteja imekuwa ndio ana kosa kulalamika? watu tunaenda na mabadiliko media ndio njia rahisi kuwasilisha malalamiko au maridhisho ya huduma. Airport muwe makini ktk huduma nzuri sio kulaumu mteja anapodhulumiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad