Al Qaeda Wamefanya Shambulio Kaskazini mwa Mali na Kuwaua Walinda Amani 10 wa UN

Al Qaeda Wamefanya Shambulio Kaskazini mwa Mali na Kuwaua Walinda Amani 10 wa UN
Wapiganaji wa kiislamu wenye mafungamano na Al Qaeda wamefanya shambulio kaskazini mwa Mali katika kambi ya Umoja wa Mataifa na kusababisha vifo vya Walinda amani 10 raia wa Chad.


Wapiganaji hao wamesema shambulio hilo wamelifanya kujibu ziara ya Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu nchini Chad, na pia uamuzi wa Rais Idriss Deby kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi hiyo.

Katika shambulio hilo la Jumapili, wapiganaji hao wenye msimamo mkali walitumia gari la magari ya mizigo na silaha nzito kushambulia kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko kaskazini mwa mji wa Kidal.


Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali Mahamat Saleh Annadif ameliita tukio hilo kama tendo la uhalifu.

Wanamgambo wamevishambulia mara kwa mara vikosi vya Umoja wamaatifa na Mali.

Tawi la Al-Qaeda kaskazini mwa Afrika, limesema limetekeleza shambulio hilo, vyombo vya habari vinaripoti.


Sehemu kubwa ya ardhi kaskazini mwa Mali zimedhibitiwa na wapiganaji Jihadi tangu 2012 hadi waliposukumwa nyuma katika operesheni ya kivita mwaka uliofuata.

Zaidi ya maafisa 15,000 - wakiwemo raia - walitumwa kama sehemu ya ujumbe wa Umoja wa mataifa, Minusma.

Lakini sehemu za nchi hiyo bado hazijadhibitiwa na serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad