Algeria Kununua Korosho ya Tanzania

Algeria Kununua Korosho ya Tanzania
Nchi ya Algeria ipo tayari kununua korosho kutoka nchini Tanzania, hili linatokana na jitihada za serikali katika kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nje ya nchi.

Hayo yamebanishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria, Saad Belabed.

Dkt. Ndumbaro amesema mazungumzo hayo ni moja ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuwakomboa kiuchumi Watanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo,  Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad