Alichokisema Diamond Platnumz Baada Ya BASATA Kuwafungulia....Kagusia Pia Tamasha la Wasafi Festival

Alichokisema Diamond Platnumz Baada Ya BASATA Kuwafungulia....Kagusia Pia Tamasha la Wasafi Festival
Msanii wa Muziki, Diamond Platnumz ameshindwa kutoa kauli ya moja kwa moja kama tamasha la Wasafi Festival Dar litafanyika au la.

Diamond na Rayvanny Walifungiwa kujihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana  baada ya kutoa Wimbo wa Mwanza, ambao haukuwa na maudhui mazuri. Tamasha la Wasafi Festival nalo lilifutwa pia.

Akiongea na Wasafi TV, Diamond amesema kuwa hawezi kutoa kauli yoyote kwasasa kama afanye au asifanye huku akieleza kuwa mpaka wakae na Team aone maoni yao.

"Siwezi kusema kauli yoyoe kama itafanyika au itakuja nyingine Wasafi Festival 2019 kwasababu lazima nikae na Team, Bodi watoe maoni yao kama inafanyika au haifanyiki ila kwa mimi nimewamisi watu wangu wa Dar Es salaam kuwafanyia kitu kikubwa na kiukweli Wasafi Festival ya Dar tulikuwa tumeipania sana," amesema Diamond Platnumz Wasafi Tv.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad