Aliyejeruhiwa ubongo kulipwa Bilioni 1

Aliyejeruhiwa ubongo kulipwa Bilioni 1
Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru Hospitali ya Nairobi kulipa fidia ya zaidi ya bilion 1 kwa mgonjwa aliyepata tatizo la ubongo baada ya Madaktari kukosea kufanya upasuaji.


Wazazi wa kijana huyo waliishtaki hospitali hiyo kwa niaba ya kijana wao ambaye kwa wakati alipofanyiwa upasuaji alikuwa mwanafunzi wa shule ya St. Mary’s High School.

Aidha Jaji wa Mahakama Kuu, George Odunga aliyekuwa akishughulika na shauri hilo pia ametoa amri ya malipo ya Tsh. Milioni 23 kwa wazazi Mgonjwa huyo.

Wazazi wa kijana huyo wamedai kwamba kijana wao asingepata matatizo hayo kama mashine hizo zingekuwa katia hali nzuri.

Malipo hayo yote yatalipwa na Dkt. Praxedes Mandu Okutuyi akishirikiana na Hospitali ya Nairobi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad