Aliyekuwa meneja wa Harmonize, Mr Puaz amejikuta akishambuliwa mtandaoni na mashabiki wa muimbaji huyo baada ya kueleza kwamba ameachana na msanii huyo baada ya pesa kumbadili tabia.
Meneja huyo alidai wakati akianza kazi na Harmonize alikuwa ni kijana mstaarabu lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga, mwanamuziki huyo aliyekiri kuwa anajituma alianza kubadilika suala alilodai kuwa huenda ni kutokana na mafanikio aliyoyapata na kwamba hana kinyongo naye na wala nia ya kumchafua.
”Naelewa kwamba ni kijana mdogo ambaye ametoka katika familia masikini, lakini utajiri na umaarufu aliopata kutokana na mafanikio ya muziki wake umeathiri tabia yake.
Mashabiki katika mitandao ya kijamii, wameanza kumshambulia meneja huyo huku wakienda mbali zaidi kumtaka aeleza sababu zilizomfanya aondoke wa muimbaji huyo. Haya ni maoni ya mashabiki.
Aliyekuwa meneja wa Harmonize, Mr Puaz ashambuliwa kisa kauli ya ‘pesa imem-badili tabia Harmonize’
0
January 05, 2019
Tags