MSANII na Video Queen wa Bongo, Muscat Abubakary ‘Amber Rutty’ baada ya kufunga ndoa hivi karibuni ameweka wazi dhamira yake ya kumzalia mumewe, Said Mtopali na kwamba jambo hilo halitachukua muda mrefu.
Amber aliiambia Showbiz kuwa anatarajia kuzaa watoto wengi na mapema kabla ndoa yake haijaanza kuingia dosari na katika kulitimiza hilo, ameshaanza mchakato.
“Napenda watoto na nitamzalia watoto wengi mume wangu mpaka kizazi kitakapoisha, namuomba Mungu anijaalie kile ninachokipanga kiweze kutimia,” alisema Amber Rutty.