Arsenal Wakabidhiwa Man Utd, Kombe la FA

Arsenal Wakabidhiwa Man Utd, Kombe la FA
Arsenal wamepangwa kukutana na Manchester United uwanjani Emirates katika raundi ya nne ya Kombe la FA.

The Gunners wanashikilia rekodi kwa kushinda kombe hilo mara 13, nao United ndio wanaowafuata wakiwa wameshinda mara 12.

Klabu ambayo haichezi soka ya ligi, Barnet, ambayo ndiyo klabu ya chini zaidi katika orodha ya viwango vya ubora wa soka iliyosalia kwenye michuano hiyo, imepangwa kukutana na klabu ya Brentford inayocheza ligi ya daraja la pili, ligi ya Championship.

Wolves wazidi kushangaza miamba, wawalaza Liverpool
Klabu ya League One Gillingham, ambao waliwatoa nje Cardiff wanaocheza Ligi ya Premia katika raundi ya tatu, watakutana na klabu nyingine ya Wales watakaposafiri kucheza na Swansea City.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester City watakuwa nyumbani dhidi ya klabu ya Burnley ambao inasuasua katika ligi kuu.

Klabu nyingine za ligi kuu zitakazokutana na Crystal Palace ambao watakuwa wenyeji wa Tottenham.

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Cup, Chelsea, watakutana na mshindi kati ya Sheffield Wednesday na Luton Town uwanjani Stamford Bridge.

Wolves, ambao waliwatoa nje viongozi wa Ligi ya Premia Liverpool katika mechi iliyochezwa Jumatatu, watasafiri kukutana na mshindi kati ya Shrewsbury na Stoke.

Droo kamili ya mechi za raundi ya nne
Swansea v Gillingham
Wimbledon v West Ham
Shrewsbury / Stoke v Wolves
Millwall v Everton
Brighton v West Brom
Bristol City v Bolton
Accrington v Derby / Southampton
Doncaster v Oldham
Chelsea v Sheffield Wednesday / Luton
Newcastle / Blackburn v Watford
Middlesbrough v Newport
Manchester City v Burnley
Barnet v Brentford
Portsmouth v QPR
Arsenal v Manchester United
Crystal Palace v Tottenham

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad