Azam Yaifunga Simba Mdomo Kombe la Mapinduzi

Azam Yaifunga Simba Mdomo Yangakua Kombe la Mapinduzi
Mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC na Simba SC umemalizika kwa wekundu wa Msimbazi, Simba SC kukubali kichapo cha mabao 2-1 katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba..

Mabao ya Mudathir Hahya dakika ya 43 na Obrey Chirwa dakika ya 72 ndio yameipa Azam FC ubingwa wa 3 mfululizo. Bao pekee la Simba lilifungwa na Yusuf Mlipili dakika ya 64.

Baada ya kutwaa mara tatu mfululizo Azam FC wamekabidhiwa moja kwa moja kombe hilo na pia wameendelea kuwa mabingwa wa Kihistoria wa michuano hiyo wakiwa wamebeba mara 5.

Mara ya kwanza walichukua kombe hilo mwaka 2012 wakiifunga Jamhuri ya Zanzibar kwenye mchezo wa fainali.

Mara ya pili ilikuwa mwaka 2013 wakiifunga Tusker ya Kenya na kisha kuwafunga Simba mwaka 2017 na kutwaa ubingwa wao wa tatu.

Mwaka 2018 wakatwaa ubingwa wa 4 wakiwafunga URA ya Uganda na sasa wamewafunga Simba na kufikisha mara tano.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad