Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB, Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny wameionyesha furaha yao baada ya msamaha kutoka katika Baraza la Sanaa Taifa Basata.
Msamaha huo wa Basata umekujaa baada ya wasanii hao kufungiwa kufanya kazi ya sanaa ndani na nje ya Tanzania hadi kufutiwa kibali cha Tamasha lao la Wasafi Festival.
Chanzo hasa cha kufungiwa ilikuwa ni wimbo wa Mwanza ambao ulikuwa na maneno yasiyokuwa na maadili, na baada ya kufungiwa wimbo huo Msanii Rayvanny aliweza kuurudisha kwenye mitandao ya kijamii baada ya wimbo huo kukataliwa kuwekwa kwenye mtandao wowote, hapo ndipo Basata walipoongeza adhabu na kuwapiga faini ya milioni 9.
Mbali na hilo wasanii hao waliweza kuutumia tena wimbo huo kwenye tamsha lao ambalo lilifanyika mkoani Mwanza mbali ya kukataliwa kuutumia wimbo huo, kitendo hicho pia kilisababisha adhabu kuongezeka na mwisho wake wasanii hao walifungiwa kufanya kazi yeyote ya sanaa ndani na nje ya nchi lakini pia kufutiwa kibali cha kufanya tamsha lao la wasafi festival ndani na nje ya nchi lakini baada ya siku kadhaa adhabu ya kutokufanya tamsha nje ilifutwa na sasa wamefutiwa adhabu yote kabisa.
kupitia ukurasa wa Instagram wa Diamond ameonyesha furaha hiyo na kuandika kuwa “Happy Independace” na kuonyesha baadhi ya clip fupi za video wakiwa studio wakirekodiwimbo mwingine na Rayvanny tena.