Baba Diamond Aomba Kuhalikwa Harusini

Baba Diamond Aomba Kuhalikwa Harusini
Baba wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa kuna tetesi zinazosambaa kuhusu mtoto wake wa kuje Diamond Platinum kufunga ndoa ingawa hajazipata kutoka kwa mhusika lakini anachosikia ni kutoka katika mitandao tu.

Hata hivyo baba huyo anasema kuwa hana kinyongo na swala hili ingawa anatamani sana kuhudhuria katika harusi hiyo lakini hawezi kwa sababu hajaalikwa lakini anaomba sana kualikwa katika harusi hiyo kwa sababu yule ni mtoto wake wa kiume.

Baba huyo na Diamond pamoja nakwamba wamekuwa na uadui lakini yeye hana kinyongo na mtoto wake kila mara amekuwa akiongea na kumtakia mema Diamond ingawa kwa upande wake hataki kabisa kuongelea chochote kuhusu baba yake.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad