Barnaba Asema Kwanini Ameamua Kuimba Gospel


Msanii wa Bongofleva Barnaba Classic, ameamua kuimba muziki wa Injili na ameachia 'EP' yenye nyimbo 6 ambayo ameshirikiana na msanii mwingine Damian Soul.

Barnaba amesema wazo la kufanya 'EP' hiyo lilitolewa na mpiga picha maarufu Michael Mlingwa maarufu kama MxCarter baada ya kupitia matatizo ya kukaa rumande kwa siku kadhaa.

''Mtu aliyetoa wazo hili kuu MxCarter tunasema asante, wazo lilikuja alipopata matatizo na kukaa rumande pale 'Central' kwa siku 8'', amesema Barbana.

Licha ya kutoa EP hiyo yenye nyimbo kama Asante, Bado muda, Amina, Hakika, Celebrate Jesus na Mesaya lakini Barbana amethibitisha kuwa ataendelea kufanya Bongofleva na hivi karibuni ataachia kazi yake inayoitwa Washa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad