Benki ya NMB yawa kinara kuchangia maendeleo



Benki ya NMB imeshika nambari moja kwa kuchangia maendeleo nchini, ambapo kwa mwaka 2018 ilitenga zaidi ya  shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuchangia jamii na  kusaidia sekta ya afya na elimu.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Ziwa Abraham Augustino baada ya kukabidhi mabati yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 20 katika vituo vya afya vya Inzidabo, Soswa, Kisaba na Iligamba,  alisema kuwa msaada huo ni mkubwa kwani vituo vya afya na elimu bado ni changamoto.

Augustino alieleza kuwa wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa kusaidia jamii, kwani jamii ndio imeifanya benki hiyo kuwa kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini.

"NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi ambapo hadi sasa ina zaidi ya matawi 228, ATM zaidi ya 800 na Wakala zaidi ya 6,000 pamoja na wateja zaidi ya milioni ambayo ni hazina kubwa ukilinganisha na benki nyingine nchini," alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole, aliishukuru benki hiyo kwa ushirikiano walioutoa kwa jamii na kuwaomba benki hiyo kuongeza matawi hadi vijijini kwani wakulima wanapata taabu pale wauzapo mazao kutokana na kutokuwa na sehemu salama ya kuhifadhia fedha zao.

Aidha Mkurungenzi wa Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda, alisema kuwa benki hiyo haijawai kuwaangusha kwani wamekuwa wakitoa msaada  mkubwa kwa jamii hasa wakati wa majanga na shughuli  mbalimbali za maendeleo ya jamii ikiwemo afya na elimu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad