Biashara za Kifamilia ni Ngumu na zinaweza Kusambaratisha Familia Nzima

Sehemu ninayofanya kazi tuliwahi kufanya kazi na kampuni fulani ya usafirishaji na utoaji mizigo bandarini, kampuni hii ilikuwa ikiendeshwa kifamilia..yaani unakuta mmiliki ni babu, meneja mkuu ni baba, rasilimali watu ni shangazi, mhasibu ni mpwa, mkuu wa madereva ni binamu n.k

Kampuni hii ilinivutia maana inaiweka familia karibu, mnakuwa mpo pamoja muda wote na pia inatoa ajira kwa wanafamilia na kutunza legacy ya mzee kama ikiendelea vizuri baada ya yeye kufariki.

Ila baadae nikaja kugundua biashara hii ina changamoto nyingi sana ukiacha changamoto za kawaida za biashara kama mabadiliko ya kiuchumi na ushindani wa soko

1.Kwanza hii biashara inakuweka njia panda mara nyingi.. Kuna mahusiano ya kibinadamu kati ya wanafamilia, mahusiano haya yanakuwa kikwazo kwa wanafamilia ku maintain mahusiano ya kikazi (professional relationship) ama ukiendekeza professionalism sana utakuta mahusiano yako na familia yanadorora, mfano kama mtu wa chini yako akifanya kosa unakuwa ngumu kumchukulia hatua sahihi za kumuwajibisha

2.Kingine wafanyakazi wengi ambao sio wanafamilia watakua wakitafuta kazi sehemu nyingine sababu wanaona kampunibni ya familia na hawana nafasi kubwa sana ya kufanikiwa wakiwa hapo

3.Ila kama wewe ni mwanafamilia inakua ngumu kuondoka kutafuta kazi sehemu nyingine na kuiacha kampuni ya familia, hasa inapokuwa matatizoni..Utaonekana ni msaliti

4.Kunakuwa na kufanya kazi kwa mazoea na kunakuwa hakuna mawazo mapya kwani wanafamilia huwa wana "take for granted" fursa wanazopewa hasa ukizingatia hawawajibishwi ipasavyo wanapokosea


5.Pia ikitokea mmiliki akifariki ghafla na hakuandaa mrithi kabla, kumtafuta mrithi wake inaweza ikaleta tabu kwani siasa za kifamilia kwenye mbio za urithi zinaweza kupelekea vita na familia kuvurugika

6.Kunakuwa pia na shinikizo la kuwaajiri wanafamilia wengine zaidi hata kama hawana vigezo bora kuliko ambavyo ungevipata ungeajiri mtu mwingine

So biashara hizi ni ngumu mno hasa ukiwa na wanafamilia ambao sio waelewa, ni bora kuwatafutia ajira kwingine kuliko kuwaleta kwenye biashara yako
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad