Binadamu wa dhahabu kuzikwa tena, baada ya kufukuliwa miaka 50 iliyopita

Binadamu wa dhahabu kuzikwa tena, baada ya kufukuliwa miaka 50 iliyopita
Kazakhstan itazika tena mabaki ya mwili wa shujaa wa kipekee katika hifadhi ya kihistoria kwa ajili ya watu wa baadae. Matumaini yao ni kwamba vizazi vya baadae watafanikiwa kugundua asili ya mtu huyo.

Wanahistoria waligundua mabaki hayo yakiwa yamembatana na silaha za dhahabu safi pamoja na sanaa mbali mbali za thamani wakati wakichimba katika makaburi ya Issyk kusini mwa nchi hiyo mwaka 1969, na hapo hapo wakampa jina la "binadamu wa dhahabu".

Tangu uhuru mwaka 1991 amekuwa ni ishara ya urithi wa asili wa taifa huko Kazakhstan. Silaha yake ya dhahabu imekuwa ni kitu cha kujivunia na imehifadhiwa katika hifadhi ya taifa ya Astana, pia hudhuru sehemu mbali mbali duniani kama alama ya tamaduni ya Kazakh.

Mifupa ya Mtu wa dhahabu imehifadhiwa katika boksi lililo kingwa na karatasi za picha.
Lakini ni machache tu yanajulikana kuhusu shujaa huyo, huku watafiti wakishangazwa na utajiri wa vito vya dhahabu walizo kuta na kwa kiasi kikubwa wakaachana na mabaki ya mtu.


Mifupa ilipatikana tena hivi karibuni katika taasisi ya upelelezi wa mambo ya kale, yakiwa yamehifadhiwa katika boksi huku yakiambatanishwa na karatasi iliyo andikwa "The Golden Man, May He Rest in Peace", yaani "Binadamu wa dhahabu, apumzike kwa amani."

"Tunajua umri wake na maisha yake ya kijamii, wakati kipimo cha vinasaba kinaweza tupatia taarifa nyingi kupita kiasi," mtafiti Dosym Zikiriya anaiambia Kazakh TV.

Lakini Yermek Zhasybayev wa hifadhi ya Issyk ametoa matumaini kidogo sana juu ya upatikanaji wa taarifa. "Mifupa ipo katika hali mbaya. Imehifadhiwa katika box kwa miaka 50 sasa na imekuwa ikikumbana na kila aina ya kakteria na virusi vikiwemo virusi vya sasa. Kwa sasa ni ngumu kupata taarifa sahihi za vina saba - ila kama tungalikuwa na fuvu au walau jino moja," amekiambia kituo kimoja cha televisheni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad