Bongo Fleva ya Zamani Tulikuwa Tunapewa Story.. Siku Hizi Tunapewa Nini?
0
January 18, 2019
Nakumbuka muziki wa kizazi kipya wa nyumbani hapa Tanzania.. around miaka ya 99 mpk 2000 na kenda... Ilikuwa ukiskia muziki unahit, basi ni kwa sababu una story.. Yaani style ya uandishi na hata kuimba/kurap ilikuwa ni story-telling..
Unakuta msanii anaandika kuhusu mwenendo wa tabia za mtu fulani (fiction).. Ambaye labda alianza kuwa kijana mwema... akaharibikiwa... au mkasa fulani.. simulizi yake sasa ndio daah mpaka raha..
Nakumbuka story ya Barua.. Story ya Aseme.. Story ya Sister sister.. Story ya Jinsi Kijana... Story ya Boss.. Story ya salome... Ya leah.. Story story...
Style hiyo naikosa kwenye miziki ya awamu hii.. wimbo mmoja unakuta una story kibao ndani yake.. unakuta kiitikio tofauti kabisa na verses... ladha inakuwemo lakini haidumu... inachosha..
Shime wanamuziki.. tuushape muziki.. tuchanganye ikibidi... Nilimwona Jay Moe akifanya story telling hivi karibuni kwenye wimbo wake wa Story za watu 3... Ilikuwa poa sana..
Natamani siku zirudi nyuma.. Kama haiwezekani, basi wazee wenzangu humu tukumbushane mistari ya nymbo za zamani ambazo zina stories nzuri..
By Interest
Tags