Breaking News: Rais Magufuli Afanya Mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri, Balozi na Makatibu Wakuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Januari, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.


Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu wa kusimamia uwekezaji ameteuliwa Angela Kairuki na atasimamia Uwekezaji.

Rais pia amemteua Dotto Biteko kuwa Waziri Kamili wa Madini.

Naye Nyongo kateuliwa kuwa Naibu Waziri madini.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu, Rais Kateua Makatibu wakuu wanne

Katibu mkuu Tamisemi ni Joseph Nyamhanga amechukua nafasi ya Yombe

Katibu mkuu Wizara ya Afya ameteuliwa Zainab Chaula, kabla ya uteuzi alikuwa TAMISEMI.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ameteuliwa Elius Mwakalinga

Sera na uwekezaji kateuliwa Doroth Mwaluko

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMU ameteuliwa Doroth Gwajima

Naibu Katibu Mkuu Utumishi ameteuliwa Francis Michael wa chuo kikuu UDSM

Nafasi ya Naibu katibu mkuu ulinzi imefutwa.

Rais amemteua Dr. Mpoki kuwa Balozi, kituo chake kitatangazwa baadae. Kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya

Rais amefungua ubalozi wa Tanzania nchini Quba

Rais amemteua Dr. Faustine Kamuzora kuwa Katibu Tawala mkoa wa Kagera, amechukua nafasi Diwani Athumani aliyeteuliwa TAKUKURU.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad