Bulaya Atoa ya Moyoni Kuhusu Kujihudhuru WaziriSAz

Bulaya Atoa ya Moyoni Kuhusu Kujihudhuru Waziri
Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ameendelea kushikilia msimamo wake wa kumtaka kujiuzulu kwa Waziri Jenister Mhagama kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Rais Magufuli juu ya hatma ya kikotooo kwa

wafanyakazi ambao ni wastaafu.

Kwa mujibu  Bulaya, suala la kikokotoo limepelekea kushuka kasi ya utendaji kazi kwa baadhi ya taasisi nchini, lakini amedai suala hilo lilikuwa likipigiwa kelele na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wakiwemo wabunge.

"Hili jambo si sawa, tunatengeza mazingira ya kuwalinda wanasiasa. Kwahiyo Rais Magufuli amfukuze kazini au Waziri mwenyewe ajiuzulu kwa sababu yeye ndiye aliyetunga hizi kanuni," amesema Bulaya.

"Viongozi tuwe na utaratibu wa kukiri tunapokosea kwasababu mchakato wa sheria huwa unaanzia mbali sana, Waziri alikuja kukisema bungeni ambacho kilijadiliwa na kwenye baraza, kwahiyo ni bora angewawajibisha wote na si mtendaji peke yake," ameongeza Bulaya.

Hii ni mara ya pili kwa Mbunge huyo wa Bunda Mjini kutaka Waziri Jenister Mhagama kutoka kwenye nafasi yake ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kuahirisha matumizi ya kanuni mpya.


Exclusive: Fire Waist By Skales!
Lit360.Africa
|
Sponsored
Want to learn a new language in 2019? - This app gets you speaking in 3 weeks
Babbel
|
Sponsored
This Drone Is The Most Amazing Invention of 2018. The Idea is Genius!
Dronex Pro
|
Sponsored
Virtually Indestructible Drone Takes Tanzania, United Republic Of By Storm
Dronex Pro
|
Sponsored
This Is How You Can Fix Your Sleeping Problems With Science
Addsolute
|
Sponsored
Polisi yakanusha mtoto kuwekwa Kabatini | East Africa Television
Wakati binti wa kazi akieleza jinsi mwanaye mwenye umri wa miezi mitano alivyofungiwa kabatini na mwajiri wake mkoani Dodoma tangu alipozaliwa, Jeshi la Polisi mkoani humo limekanusha madai ya mtoto huyo kufungiwa kabatini, na kusema kuwa mtuhumiwa wanamshikilia kwa usalama wake,
EATV

TOP STORIES

SPORT
“Shughuli ya Lechantre imekwisha”-Manara

SPORT
Ngoma ashindwa kuichezea Azam, Kagame

CURRENT AFFAIRS
Amuua mke mwenza na kumzika shambani

CURRENT AFFAIRS
Mbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM



MOST POPULAR

ENTERTAINMENT
Msanii wa filamu afariki dunia

ENTERTAINMENT
WanaHip Hop wahoji elimu ya Nikki wa Pili

CURRENT AFFAIRS
Polisi yakanusha mtoto kuwekwa Kabatini

CURRENT AFFAIRS
Kaburi lafukuliwa, Sanda yachomwa moto

SPORT
"Hatukuwa na malengo mwaka 2018" - Mwinyi Zahera
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2018 East Africa Television Limited. All Rights Reserved

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad