Bunge lasitisha kufanya kazi na CAG, Spika Ndugai aeleza


Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad. 

Kutokana na hali hiyo amewataka wajumbe wa kamati za Bunge za PAC na LAAC kufanya kazi katika kamati nyingine. 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya CAG kutoa kauli na kueleza kuwa Bunge kimekuwa dhaifu na kutakiwa ufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujieleza. 

Utakumbuka hivi karibuni CAG alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kusema,'Kama tunatoa ripoti zinaonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, hupo kwangu ni udhaifu wa Bunge,'. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad