CCM Yamkana Cyprian Musiba "Hatujawahi Kumtumia Yale Ni Maoni Yake Binafsi"

CCM Yamkana Cypoan Musiba "Hatujawahi Kumtumia Yale Ni Maoni Yake Binafsi"Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefunguka na kueleza kuwa hakijawahi kumtuma Cyprian Musiba kuzungumza chochote.

Hayo yameelezwa na Katibu Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole kwenye mahoajiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV.

Polepole amesisitiza kwamba yale ni maoni yake binafsi na CCM haihusiki naye, huku akishauri watu ambao wanaguswa na tuhuma zinazotolewa na Musiba kwenda Mahakamani na kufuata taratibu za kisheria.

Utakumbuka kuwa Cyprian Musiba ambaye anajinasibu kama 'Mwanaharakati' amekuwa na kawaida ya kutoa tuhuma dhidi ya viongozi mbalimbali ndani ya chama hicho na vile vya upinzani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad