Chelsea imemsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain mpaka mwisho wa msimu.
Miamba hiyo ya London pia ina nafasi ya kumsajili moja kwa moja kwa kima cha pauni milioni 31.3. Kuna uwezekano pia wa kuongeza mkataba huo wa mkopo mpaka Juni 2020 lakini itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 15.
Higuain, 31, ambaye ni raia wa Argentia amecheza nusu ya kwanza ya msimu huu kwa mkopo katika klabu ya AC Milan, na kufunga magoli nane kwenye michezo 22.
"Ni timu ambayo nimekuwa nikiipenda na ina historia pana, uwanja mzuri na inashiriki Ligi ya Premia ambayo nimekuwa niiitamani kila siku kuicheza."
Kutokana na usajili huo kufanyika baada ya saa sita usiku ya Jumatano, Higuain hataweza kuichezea klabu yake mpya kwenye mechi ya nusu fainali ya pili ya Kombe la Corabao usiku wa leo dhidi ya Tottenham.
"Ni mshambuliaji mwenye nguvu, alidhihirisha hilo katika msimu wangu wa kwanza na Napoli," amesema Sarri. "Alifanya vizuri mno. Kwa hakika, yeye ni moja ya washambuliaji magwiji zaidi ambao nimewahi kufanya nao kazi.
Boateng ajiunga na Barcelona
"Ninaamini ataanza tena kushinda na timu yetu. Najua amekubwa na ukame kwa sasa."
Higuain ameongeza kuwa: "Sasa nina imani nitaweza kuilipa Chelsea uwanjani kwa imani walioinesha kwangu. Nina hamu kubwa ya kuanza kucheza na naamini nitazoea mazingira kwa haraka iwezekanavyo."
Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia amesema Higuain ndio alikuwa kipaumbele chao cha kwanza katika dirisha la usajili la mwezi Januari na amewasilia kiwa na "rekodi iliyodhihiri (ya kucheza) katika kiwango cha juu".
Kocha Sarri na Higuiain walikuwa na msimu bora pamoja na Napoli mwaka 2015/16 na sasa wameungana tena Chelsea.
"Ameshafanya kazi hapo awali na Maurizio kwa ufanisi mkubwa na anajua kocha wake anapendelea mchezo wa aina gani," ameongeza Granovskaia.
"Huu haukuwa usajili mwepesi kwetu sababu kulikuwa na wahusika wengi, lakini tunafuraha kuona kuwa tumeweza."
Higuain alihushwa na tetesi za kuhamia klabu ya Arsenal kabla ya Juventus kumsajili kwa dau liloweka rekodi nchini Italia la pauni milioni 75.3 akitokea Napoli Julai 2016.
'Watanzania, hawasubutu kuzungumza' aambiwa rais Magufuli
Baada ya kucheka na nyavu mara 40 kwa misimu miwili na Juventus, alihamia AC Milan kwa mkopo mwezi Agosti. Kulikuwa na fursa kwa Milan kumbakisha mwisho wa msimu huu kwa dau la pauni milioni 36.
Alianza kwa kiwango cha juu maisha yake na Milan kwa kufunga magoli sita katika mechi tano za mwanzo, hata hivyo amefunga goli moja tu kwenye michezo 12 iliyopita.
Chelsea kwa sasa ipo katika nafasi ya nne katika msimao wa Ligi ya Premia, wakiwa na alama tatu juu ya mahasimu wao Arsenal ambao waliwafunga 2-0 siku ya Jumamosi.