Katika hali ya mshangao unaambiwa Mwanachama mmoja wa Yanga jana alivaa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Omar Kaya akielezea alihusika katika kumuangusha Kocha Mwinyi Zahera.
Hali hiyo iliyoleta taharuki mpaka ngumu kutaka kurushwa ni kutoka na usajili wa kipa aliyetoka Mawenzi Market, Ibrahim Hamid kusainiwa na Yanga bila matakwa ya Zahera.
Kwa mujibu wa Radio One, Mwanachama alimvaa Kaya huku akieleza alihusika katika upigaji wa fedha na kushindwa kusajili kwa mujibu wa maagizo ya Kocha Mkuu.
Alisema kuwa Kaya na Nyika walishirikiana kusajili mchezaji huyo ambaye ameonesha kiwango duni kwenye mashindano ya Mapinduzi CUP huko Zanzibar.
Aidha, Mwanachama huyo alisema uhakika wa Kaya juu ya upigaji wa fedha za Yanga huku akimtaja Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika kuwa alishirikiana naye, ni kuwa walipewa taarifa na kiongozi wa juu ambaye ni Siza Lyimo.
Tukio hilo lilimalizika kwa baadhi ya watu waliokuwa karibu kulisuruhisha na baada ya majibizano na kauli nzito zilizokuwa zikitoka pande mbili kuzidi mpaka ngumikukaribia kurushwa.