Dereva Aliyeng’atwa na Trafiki Mkoani Songwe, Aburuzwa Mahakamani Kwa Makosa Mawili
0
January 15, 2019
Kuanzia juzi kulikuwa na video iki-trend kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Dereva wa Fuso akipambana na Askari wa Usalama wa Barabarani, huku akilalamika kuwa anang’atwa na Askari huyo.
Sasa kufuatia tukio hilo, tayari Jeshi la Polisi mkoani Songwe limeeleza sababu ya askari wa usalama barabarani kumshambulia dereva huyo kwa kwa kumpiga.
Jeshi la Polisi mkoani humo limesema kuwa, Dereva huyo alitumia lugha ya matusi na kutotii amri .
Akiongea kwenye kipindi cha Alasiri cha Clouds TV, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, Yusuph Sarungi amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi Januari 12, 2019 saa 2:30 asubuhi katika eneo la Transforma, halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba wakati askari hao wakishirikiana na maofisa toka Sumatra wakiwa kwenye ukaguzi wa magari mbalimbali.
Kamanda Sarungi ametaja jina la dereva huyo kuwa ni Mawazo Jairos (29) mkazi wa Mbeya na alikuwa anaendesha gari aina ya Mistubishi Fuso, lenye namba za usajili T842 AAC.
Kwa upande mwingine, Kamanda Sarungi amesema kuwa Dereva huyo leo Januari 14, 2019 ameburuzwa mahakamani kujibu mashtaka mawili ya kuzuia askari kufanya kazi yao na kumjeruhi Askari .
Tags