Diamond Aeleza Kwanini Walitumbuiza Wimbo uliofungiwa na Basata
0
January 05, 2019
Msanii wa muziki Bongo Fleva, Diamond ameleza ni kwanini walitumbuiza wimbo wa 'Mwanza' ambao tayari ulikuwa umefungiwa.
Muimbaji huyo kutoka WCB akizungumza na Wasafi TV amesema kuwa walilazimika kufanya hivyo mkoani Mwanza wakati wa tamasha la Wasafi Festival kutokana na uhitaji kuwa mkubwa.
"Unajua mimi ndio nilikuwa naomba sana, halafu Mwanza walikuwa wanaomba huo wimbo sana, hadi watu anatingisha jukwaa, sasa tukaangalia ushafika muda kama saa tisa watoto hamna, watu wamelala ikabidi tuamshe ili mashabiki wasione tunawaletea pozi," amesema Diamond.
Wimbo Mwanza maarufu kama Nyegezi ambao ni wa Rayvanny akimshirikisha Diamond,umefungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutokana na kukiuka maadili.
Tags