Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka kuhusu mipango yake ya kuoa.
Diamond akizungumza na Wasafi TV amesema kuwa tarehe waliyopanga awali kwa ajili ya ndoa wameisogeza mbele kutokana anataka harusi yake iwe nzuri na kuhudhuriwa na watu wengi.
"Ndoa yangu ilitakiwa iwe siku ya Valentine tarehe 14 lakini tumeipeleka mbele. Watu wengi wanatakiwa kuja kuhudhuria kwa sababu ndoa yangu watakuja kina Rick Ross," amesema Diamond.
Kwa sasa Diamond Platnumz yupo mapenzini na mrembo Tanasha kutoka nchini Kenya, bado haijajulikana iwapo atamuoa mrembo huyo.