Diamond Platnumz utakuja kuoa mganga wa kienyeji - Masanja



Mchungaji mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji  ametoa ushauri kwa Mwanamuziki Maarufu nchini, Diamond Pltanumz kuoa mapema kwani akichelewa anaweza kuoa mganga wa kienyeji.

Masanja amesema kuwa watu wajiulize kila mtu anayetaka kuolewa na Diamond anasema mara analoga familia, hivyo amemtaka kuoa mapema ili kuepuka kuja kuoa mdada anayenuka mitishamba.

"Diamond Platnumz oa mapema utakuja kuoa mganga wa kienyeji, wewe jiulize hivi kama wewe huoi sasa hivi nimesikia kila mdada anayetaka kuolewa leo na Diamond nimesikia eh wananiloga na wanaloga familia kama mdada wa kwanza unaenda naye alafu humuoi, pili nae humuoi, watatu mwisho wa siku utaoa kadada kanako nuka mitishamba, Oa mapema ndugu yangu unangoja nini?, Masanja ameiambia Wasafi Tv.

Diamond Platnumz kwasasa anatoka kimapenzi na Natasha kutoka nchini Kenya, ambapo mpaka sasa haijajulikana kama atamuoa mrembo huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad