Baada ya ndoa ya wasanii wawili bongo Irene Uwoya na Dogo Janja kuingia doa na kufikia hatua ya kurushiana vijembe mitandaoni, baba mlezi wa Dogo Janja, Madee Ali 'Seneda' ameingilia kati suala hilo.
Akizungumza na www.eatv.tv, Madee amesema kwamba alishtushwa na tukio la Irene na Dogo Janja kuanza kurushiana vijembe, na kuamua kuwakalisha chini wote wawili, akiwataka kuacha kitendo hicho.
“Nishawasema jana, mimi binafsi niliyafuatilia jana na nimeongea nao yameisha, Dogo Janja pia nilishaongea naye halitojirudia na wala hutoona tena”, amesema Madee.
Wawili hao walianza kurushiana maneno ya mafumbo katika mtandao wa instagram jana Januari 07, baada ya kudhihirisha wazi juu ya kufa kwa ndoa yao ambayo haijamaliza hata mwaka.