Ebitoke Aliponda Penzi la Ben Pol na Anerlisa "Analelewa Tu Hamna Cha Zaidi"

Ebitoke Aliponda Penzi la Ben Pol na Anerlisa "Analelewa Tu Hamna Cha Zaidi"
Mchekeshaji Ebitoke ameponda vikali mahusiano ya Ben Pol na mrembo Anerlisa kutoka nchini Kenya.Utakumbuka Ebitoke aliwahi kugonga vichwa vya habari vilivyo kwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Ben Pol.

Akizungumza na Wasafi TV amesema anamuona Ben Pol kama mwanaume anayelelewa tu hakuna zaidi ya hapo.

"Mimi sijisikii vibaya kwa sababu yule namuona kama kibenteni ninabaki nacheka, mtu unakula bata, unapelekwa Dubai kwa hela gani, wewe siunalelewa mbeba pochi tu," amesema Ebitoke.

Kipindi cha nyuma mahusiano ya Ben Pol na Ebitoke yaliwapa raha wapenda udaku kwa namna alivyokuwa yakiripotiwa kila mara kwenye vyombo vya habari. Walienda mbali hata Ben Pol kumshirikisha Ebitoke kwenye wimbo wake uitwao Tuliza Boli, hata hivyo yote hayo yamebaki historia kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad