Fahamu zaidi kuhusu msiba wa muigizaji Mama Abdul


Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba, amesema msiba wa muigizaji Mama Abdul ni msiba ni pigo kwenye kiwanda kizima cha filamu Tanzania na wasanii wanatakiwa kuungana kuifariji familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.



Akiongea kwa njia ya simu na www.eatv.tv Mwakifamba amesema amepokea taarifa za msiba huo akiwa safarini hivyo hajaongea na familia juu ya chanzo cha msiba huo lakini anafanya mawasiliano usiku huu ili kujua undani wake.

''Nipo safarini ndio nimefika usiku huu, kuhusu chanzo cha kifo chake bado sijawasiliana na familia lakini niwaombe tu wasanii wenzangu tuungane katika kipindi hiki kigumu cha kumhifadhi mwenzetu kisha mimi nafanya mawasiliano na familia na nitatoa taarifa rasmi'', amesema.

Kwa mujibu wa taarifa ya mapema iliyotolewa na Kamati ya Matukio Maadili na mikataba ya Chama cha waigizaji TDFAA (M) Kinondoni na Ubungo ilieleza kuwa msiba huo umetokea mchana leo nyumbani kwake Mburahati na msiba upo hapo nyumbani.

Aidha ilifananua kuwa taarifa juu ya taratibu za mazishi itatolewa baadaye baada ya kikao na familia, huku wasanii pia wakiombwa kushirikiana.

Baadhi ya wasanii walioonesha kusikitishwa na msiba huo ni pamoja na JB, Riyama Ally, Johari, Monalisa na wengine.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad