Fatma Karume ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa nchini, kutokana na historia ya baba yake mzazi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi huku yeye akionekana kuwa karibu sana na viongozi wa vyama vya upinzani.
''Sijawahi kumiliki na wala sitaki kumiliki kadi ya chama chochote-, kuhusu kushiriki kwenye siasa naweza kushiriki bila kuwa mwanachama wa chama chochote, kwani sasa hivi nawakosoa vizuri sana kwa hiyo naweza kutoa maoni yangu hata kama wakiniita mwanaharakati." alisema Fatma Karume.
Pia amesema Kuhusu kuwa mfuasi wa chama cha siasa kwa sasa akitaka atafanya asipotaka ataacha atasema kama akimiliki kadi ya chama chochote.
Hivi karibuni alizungumzia kuonekana kwake kwenye maazimio ya vyama vya upinzani nchini Fatma Karume alisema alionekana kwenye mkutano huo baada ya kualikwa na vyama husika kutoa elimu juu ya masuala ya katiba.