Filamu ya maisha ya mwanamuziki kutoka Zanzibar yazoa tuzo nchini Marekani

Filamu ya maisha ya mwanamuziki kutoka Zanzibar yazoa tuzo nchini Marekani
Filamu ya Bohemian Rhapsody inayohusu maisha ya muimbaji kinara bendi ya Queen ya Uingereza, Freddie Mercury ambaye ni mzaliwa wa visiwani Zanzibar imenyakua tuzo mbili kubwa za tamasha la filamu la Golden Globes.

Tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo huko Beverley Hills, California nchini Marekani usiku wa kuamkia leo ambapo Bohemian Rhapsody imenyakua tunzo katika kipengele cha filamu bora ya mwaka 2018 na Rami Malek ambaye ndiye alikuwa mhusika mkuu akiigiza kama Mercury amenyakua tunzo ya mwigizaji bora wa kiume.

Filamu nyengine zilizoshinda tunzo ni A Star Is Born ambayo ilipendekezwa sana lakini iliambulia tunzo moja tu. Huku filamu ya Green Book ilikua ni moja kati ya filamu kubwa zilizong'aa baada ya kung'oa tunzo tatu za filamu bora ya kuchekesha, mwigizaji bora msaidizi iliyoenda kwa mwigizaji Mahershala Ali na filamu iliyoandikwa vizuri zaidi.


Mahershala Ali huko nyuma aliwahi kupendekezwa katika tunzo za Golden Globes kwa uhusika wake kwenye filamu ya Moonlight
Ushindi wa Bohemian Rhapsody unakuja kwa kishindo ijapokuwa kulikuwa na vikwazo vingi wakati wa utayarishaji wake.

Muongozaji Mkuu wa awali wa filamu hiyo Bryan Singer alifukuzwa kazi kutokana na kile kilichotajwa kuwa "tabia zisizovumilika" na kuibua taarifa kuwa alikua na mifarakano na Malek wakati wakiandaa filamu. Dexter Fletcher akaletwa ili kumaliza utayarishaji wa filamu hiyo.

Filamu hiyo imevuma sana na kufanya vizuri katika mauzo sokoni na sasa jina la Malek litaingia katika majina pendekezwa ya tunzo maarufu zaidi za Oscar baadae mwezi huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad