Flaviana Matata Foundation imetoa vifaa kwa wanafunzi 284 vya kujifunzia

Taasisi ya “Faviana Matata Foundation” iliyopo chini ya mwanimitindo Flaviana Matata imetoa vifaa vya kujifunzia kwa jumla ya watoto 284 waliopo katika shule za msingi nchini kwaajili ya maandalizi ya kuanza muhula mpya wa masomo kwa mwaka huu 2019 na pia taasisi hiyo imetoa vifaa kwa waalimu kwa ajili ya kuwasaidia kufundishia wanafunzi.

Flaviana ameandika >>>”Leo muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2019 umeanza. Taasisi yetu @flavianamatatafoundation ambayo ni walezi wa Shule ya Msingi Msinune tunaendelea na utaratibu wetu wa kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima”

“Kwa mwaka 2019, watoto 284 wa Shule ya Msingi Msinune kila mmoja kapata begi la shule, kalamu za wino 50 , kalamu za risasi 50 na vifutio ambavyo vitakidhi mahitaji yao kielimu kwa mwaka huku wazazi wakitimiza mahitaji mengine yaliyobaki. Upande wa walimu taasisi imetoa kalamu, chaki, rejista za masomo na karatasi (reams) kwa ajili ya kudurufu (copy) mitihani na kazi za masomo”



“Tukiongelea mafanikio ya Taasisi shuleni Msinune, mpaka mwaka jana tumefanikiwa kukamilisha ujenzi na ukarabati wa madarasa, ofisi za walimu, vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi na mradi wa maji safi.Kwa mwaka 2019-21 Tutajikita zaidi kwenye ujenzi wa nyumba za walimu shuleni kutatua changamoto ya makazi ya walimu shuleni hapo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali”

“Mafanikio ya hili yatajenga mazingira rafiki zaidi kwa walimu kufanya kazi na kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Bado tunazidi kuwaasa Watanzania kuendelea kujitolea kwa namna moja au nyingine katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini”






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad