Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, leo Alhamisi, Januari 17, 2018 ameshindwa kabisa kufika katika Mahakama ya Kisutu kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni mgonjwa.
Wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo, mbele ya hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa ambapo amedai kuwa shauri hilo wanasubiri maamuzi kutoka Mahakama ya Rufani huku Hakimu Mashauri akiahirisha kesi hiyo hadi, Januari 31, mwaka huu.
Mbowe na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake (Bawacha) Ester Matiko, wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana.
Mbowe na Matiko, walifutiwa dhamana, Novemba 23, 2018 na hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kukiuka masharti ya dhamana.
Freeman Mbowe ni Mgonjwa.... Ashindwa Kufika Mahakamani
0
January 17, 2019
Tags