Gabriel Jesus Afungia Man City Mawili na Kupunguza Uongozi wa Liverpool Kileleni

Gabriel Jesus afungia City mawili na kupunguza uongozi wa Liverpool

Gabriel Jesus alifunga mabao mawili na kuwawezesha Manchester City kuwalaza Wolves mabao 3-0 na kupunguza uongozi wa Liverpool kileleni hadi alama nne.

City hawakuweza kurejelea ufungaji wa mabao mengi ambao walikuwa wameandikisha dhidi ya Rotherham (7-0) na Burton (9-0), ambapo kwa jumla walikuwa wamefunga mabao 16.

Lakini si wengi walikuwa na shaka kwamba wangeibuka washindi, ingawa kwa mabao machache. Hata hivyo, wapo waliotarajia Wolves watoe ushindani mkali ikizingatiwa kwamba wamekuwa mwiba kwa klabu kubwa.

Jesus alianza ufungaji wa mabao dakika ya 10 pale Leroy Sane alipoifikia pasi kutoka kwa Aymeric Laporte na akamwandalia Mbrazil huyo mpira safi na kumuwezesha kufunga.

Wolves wazidi kushangaza miamba, wawalaza Liverpool
Arsenal wakabidhiwa Man Utd Kombe la FA
Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2018/19
Kibarua ambacho tayari kilikuwa kigumu kwa Wolves kiligeuka na kuwa kigumu hata zaidi pale Willy Boly alipofukuzwa uwanjani dakika ya 19 kwa kumchezea visivyo Bernardo Silva. Alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja.

City mwanzoni walionekana kutotumia wingi wa wachezaji uwanjani kujifaidi na walipata wasiwasi pale Jonny alipokaribia sana kufunga kutoka kwa pasi ya Diogo Jota, katika shambulio nadra sana la wageni.

Hilo liliwazindua City na dakika chache baadaye, wakaongeza uongozi wao kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 39.

Ryan Bennett alimwangusha Raheem Sterling eneo la habari na Jesus akafunga mkwaju waliozawadiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad