Harmonize Atoboa Siri ya Misaada Anyotoa

Harmonize Atoboa Siri ya Misaada Anyotoa
Msanii wa muziki Bongo, Harmonize amesema suala la yeye kutoa misaada hafanyi pekee yake bali kuna watu ambao anashirikiana nao kwa ukaribu zaidi.

Muimbaji huyo kutokea WCB amesema watu hao ndio wanafanya kazi kubwa kujua wahitaji mara nyingi wapo maeneo yapi.

"Nina timu ambayo inahakikisha Harmonize anakuwa vizuri kila wakati, pia kuna watu ambao huwa wanakaa nyuma yangu kujua watu fulani wanapatikana wapi na wapi," amesema.

"Hili suala lilichukua muda kidogo, wao ndio walifanya utafiti na kujua walemavu wapo hapa ndio tukaenda posta kununua baskeli baada ya kutoka Kenya," ameongeza.

Hapo jana Harmonize alitoa misaada kwa walemavu wa miguu ambao aliwapatia baiskeli, pia utakumbuka Septmber 2018 alitoa mitaji wa wafanyabiashara wadogo (machinga) kariakoo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad