Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya WCB Harmonize alimaarufu KondeBoy ametumia siku ya mwaka mpya kuwasifia na kutoa shukurani zake kwa mashabiki zake kutoka Kenya.
Msanii huyo kutoka Tanzania ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwamwagia sifa nyingi mashabiki zake kutoka Kenya na kuandika maneno haya:- ” INGAWA MIE NI MTANZANIA NA NUSU….!!! ILA NAJIVUNIA UWEPO WENU NDUGU ZANGU WA KENYA …!!!! I LOVE YOU 🇰🇪 YOU CHANGED MY LIFE 🙏 FROM TANZANIAN SINGER
TO EAST AFRICAN YOUNG STER
I LOVE YOU FROM MY HEART ❤
TULIIBADIRI TAREHE 31/12/2018
KUWA TAREHE 12/12/2018 NA TUKAIMBA HAPPY BIRHDAY KENYA…!!!! ❤ GOD BLESS 254🇰🇪 THANKS ALO NAAMINI 2019 ITAKUWA ZAIDII….!!! EAST AFRICA TO THE 🌍 ✔ “