Hatimaye G Nako Amjibu Q chief
0
January 31, 2019
Baada ya msanii mkongwe Bongo, Q Chief kueleza kuwa G Nako amekuwa akifanya kolabo nyingi sana kitu ambacho anaona kinaweza kushusha uwezo wake, hatimaye G Nako amejibu hilo.
Akizungumza na kipindi cha The Playlist cha Times FM amesema si kweli anafanya kolabo nyingi sana kwani kana kazi nyingi pia amezikataa.
"Kwanza kabisa nishakataa kolabo nyingi sana halafu kitu kingine kuna nyimbo nyingine
nashawishika kufanya kutokana nataka kufanya kitu kizuri," amesema.
G Nako amekuwa akifanya chorus karibu zote za kundi la Weusi na zimekuwa zikifanya vizuri. Ameweza kufanya kazi na wasanii kama Country Boy, Mwana FA, Jux, Belle 9, Izzo Bizness, Frida Amani na wengineo.
Tags