Hayawi Hayawi Yamekua! Tanasha Atambulisha Ukweni Bi Sandra Ampokea

Hayawi Hayawi Yamekua! Tanasha Atambulisha Ukweni Bi Sandra Ampokea
Hatimaye msanii Diamond Platnumz amemtambulisha mpenzi wake mpya, Tanasha kwa mama yake mzazi, Sanura Kassim Sandra.

Mahusiano na Diamond na Tanasha yalianza kugonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwaka jana na hata kuvishwa tetesi za ndoa. Hata hivyo wengi hawakutilia maanani iwapo muimbaji huyo atamtambulisha Bibie kwa familia yake.

Siku ya jana Diamond maarufu kama Simba akaonyesha ni kweli kakolewa kwenye penzi la Bibie Tanasha pale alipomtambulisha kwa familia yake.

Katika video ambazo Diamond amezichapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram zimeonyesha Tanasha akisalimiliana na Bi. Sandra pamoja na Dada wa Diamond, Esma Platnumz.

Tanasha ambaye ni mrembo kutokea nchini Kenya anazidi kuwa maarufu Afrika Mashariki kwa kuwa mapenzini na Diamond. Awali Bibie alijizolea umaarufu nchini mara baada ya kuonekana kwenye video ya Alikiba na Christian Bella.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad